Mbunge wa jimbo la mchinga Mh. Hamidu Bobali, anaetarajia kumaliza muda wake amepata ajali mbaya maeneo ya kijiji cha Mnimbila, mkoani Lindi. Ajali hiyo ilitokea baada ya tairi tatu za gari ilo kupasuka kwa pamoja.
Akizungumza na mwaandishi wetu wa habari Mh. Hamidu Bobali, aliwaondoa hofu wananchi kwa kuwaambia watu wote waliokuja ndani ya gari hilo ni wazima wafya.
"Tumepata ajari mbaya sana usiku huu hapa mnimbila, Kijijini katika mazingira tambalale. Taili 3 zilipasuka kwa pamoja na gari kupinduka mara 3. Watu wote waliokuwa kwenye gari ni wazima wa afya ila Gari ipo light off"