TAZAMA MATOKEO YAKO/ YA MWANAO BILA INTERNET
Sasa dunia ni kama kijiji, najua utakubaliana na mimi katika hili. Katika miaka ya hivi karibuni tumekua tukishuhudia mabadiliko mengi toka mifumo ya kianalojia kwenda kidijitali
Katika hilo pia kwenye elimu tunashuhudia mabadiliko ya namna hiyo, mfano hivi sasa tumezoea kuangalia matokeo ya mitihani taifa kwa kutumia simu janja.
Lakini kama haitoshi sasa tunaweza kupata matokeo yetu bila ya kutumia simu janja yaani kwa kutumia 'KISWASWADU' (simu isiyo na uwezo wa internet) kama inavyo elekezwa hapo chini
- Piga *152*00#
- Chagua namba 8.ELIMU
- Chagua namba 2.NECTA
- Chagua aina ya huduma 1.MATOKEO
- Chagua aina ya Mtihani 2.ACSEE
- Andika namba ya Mtihani na Mwaka Mfano:S0334-0556-2019
- Chagua aina ya Malipo (Gharama kwa kila SMS ni Tshs 100/=)
- Baada ya kukamilisha malipo utapokea ujumbe mfupi wa matokeo