1. Aanguaye huanguliwa.
2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika
guu.
3. Abebwaye hujikaza.
4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti.
5. Adui aangukapo, mnyanyue.
6. Adui mpende.
7. Adui wa mtu ni mtu.
8. Afadhali ya Musa kuliko ya
Firauna.
9. Ahadi ni deni.
10.
Aisifuye mvua imemnyea.
11.
Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
12.
Akiba haiozi.
13.
Akili ni mali.
14.
Akili ni nywele kila mtu ana zake.
15.
Akili nyingi huondowa maarifa.
16.
Akutukanae hakuchagulii tusi.
17.
Akipenda chongo huita kengeza.
18.
Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki.
19.
Akufanyiaye ubaya, mlipe wema.
20.
Akupaye kisogo si mwenzio.
21.
Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
22.
Alisifuye jua, limeuangaza.
23.
Aliye juu msubiri chini.
24.
Aliye kando, haangukiwi na mti.
25.
Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi.
26.
Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua.
27.
Akufukuzae hakwambii toka.
28.
Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa.
29.
Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga.
30.
Ana hasira za mkizi.
31.
Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga.
32.
Angurumapo simba, mcheza ni nani?
33.
Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi.
34.
Apewaye ndiye aongezwaye.
35.
Anaejipiga mwenyewe, halii.
36.
Asifuye mvuwa imemnyea.
37.
Asiye kubali kushindwa si mshindani.
38.
Asiye kujua, hakuthamini.
39.
Asiye kuwapo na lake halipo.
40.
Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu.
41.
Asiye na mengi, ana machache.
42.
Asiye na mwana abebe jiwe.
43.
Asiye uliza, hanalo ajifunzalo.
44.
Asiyejua maana, haambiwi maana.
45.
Atangaye na jua hujuwa.
46.
Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali).
47.
Atekaye maji mtoni hatukani mamba.
48.
Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
49.
Baada ya dhiki faraja.
50.
Bahari hailindwi.
51.
Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume.
52.
Bandu bandu huisha gogo.
53.
Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
54.
Bendera hufuata upepo.
55.
Biashara asubuhi.
56.
Bilisi wa mtu ni mtu.
57.
Bora kinga kuliko tiba.
58.
Bora lawama kuliko fedheha.
59.
Bora mchawi kuliko fitina.
60.
Biashara asubuhi.
61.
Bora nusu shari kuliko shari kamili.
62.
Bwawa limeingia ruba.
63.
Cha mtu mavi.
64.
Chaka la samba, halilali nguruwe.
65.
Chamlevi huliwa na mgema.
66.
Chanda chema huvikwa pete.
67.
Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako.
68.
Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza.
69.
Chombo cha kuzama hakina usukani.
70.
Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
71.
Chui hakumbatiwi.
72.
Chururu si ndo ndo ndo.
73.
Dalili ya mvua mawingu.
74.
Damu nzito kuliko maji.
75.
Daraja livuke ulifikapo.
76.
Dawa ya moto ni moto.
77.
Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea.
78.
Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya
Mungu.
79.
Dawa ya moto ni moto.
80.
Donda ndugu halina dawa.
81.
Dua la kuku halimpati mwewe.
82.
Fadhila huna, hata hisani hukumbuki?
83.
Fadhila ya nyuki ni moto.
84.
Fadhila ya punda ni mateke (mashuz)
85.
Fahari ya macho haifilisi duka.
86.
Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
87.
Fata nyuki ule asali.
88.
Fimbo ya mbali haiui nyoka.
89.
Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua.
90.
Funika kombe mwanakharamu apite.
91.
Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
92.
Gome la udi, si la mnuka uvundo.
93.
Haba na haba, hujaza kibaba.
94.
Haki ya mtu hailiki.
95.
Hakuna marefu yasiyo nan cha.
96.
Hakuna masika yaso mbu.
97.
Hakuna msiba usio na mwenziwe.
98.
Hakuna siri ya watu wawili.
99.
Hakuna ziada mbovu.
100. Hala hala mti na macho.
101. Hamadi ni ilio kibindoni, na
silaha ni iliyo mkononi.
102. Hapana marefu yasio na mwisho.
103. Haraka haraka haina baraka.
104. Haraka haraka haina baraka.
105. Haramu yako halali kwa mwenzio.
106. Hasidi hasada.
107. Hasidi mbaya.
108. Hasira, hasara.
109. Hatua ndefu hufupisha mwendo.
110. Hauchi hauchi, unakucha.
111. Hayawi hayawi, mara huwa.
112. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
113. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
114. Heri nitakula na nini? kuliko nitakula
nini?
115. Heri ya marama kuliko kuzama.
116. Hiari ya shinda utumwa.
117. Hogo halihogoki mpaka kwa hogo
jenziwe.
118. Hucheka kovu asiye kuwa na
jeraha.
119. Ila ya kikwapa, kunuka pasipo
kidonda.
120. Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo.
121. Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo.
122. Imara ya jembe kaingojee
shambani.
123. Jambo usilolijua, ni sawa na
usiku wa giza.
124. Jembe halimtupi mkuliza.
125. Jihadi ya nzi, kufa kidondani.
126. Jina jema hung’ara gizani.
127. Jini likujualo halikuli
likakwisha.
128. Jino la pembe si dawa ya pengo.
129. Jitihada haiondoi kudura.
130. Jitihadi haiondoi kudura.
131. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
132. Jungu kuu, halikosi ukoko.
133. Jununu fununu.
134. Kafiri akufaaye, si muislamu
asiye kufaa
135. Kafiri akufaye si Isilamu
asiyekufa.
136. Kama hujui kufa, tazama kaburi.
137. Kama wewe wasema cha nini, mwezio
asema nitakipata lini.
138. Kamba hukatika pabovu.
139. Kanga hazai ugenini.
140. Kawaida ni kama sheria.
141. Kawia ufike.
142. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
143. Kelele za chura hazimzuwii
ng'ombe kunywa maji.
144. Kelele za mlango haziniwasi
usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba)
145. Kenda karibu na kumi.
146. Kesho kesho, kesho kiama.
147. Kiburi si maungwana.
148. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.
149. Kichango kuchangizana.
150. Kidole kimoja hakivunji chawa.
151. Kikulacho ki nguoni mwako.
152. Kikushindacho kukila usikitie
ila.
153. Kila chombo kwa wimblile.
154. Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao.
155. Kila mlango na ufunguwo wake.
156. Kila mtoto na koja lake.
157. Kila mtu huzikwa na kaburi lake.
158. Kila mtu na bahati yake.
159. Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta
kwake.
160. Kila mtu hulilia mamae.
161. Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
162. Kila shetani na mbuyu wake.
163. Kilimia kikizama kwa jua, huzuka
kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
164. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali
wakaingia.
165. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
166. Kinga na kinga ndipo moto
uwakapo.
167. Kingiacho mjini si haramu.
168. Kinyozi hajinyoi.
169. Kinywa ni jumba la maneno.
170. Kipendacho moyo dawa.
171. Kipofu hasahau mkongojo wake.
172. Kipya kinyemi ingawa kidonda.
173. Kisebusebu na kiroho papo.
174. Kisokula mlimwengu, sera nale.
175. Kisokula mlimwengu, sera nale.
176. Kisu kimenifika mfupani.
177. Kitanda usicho kilalia hukijui
kunguni wake.
178. Kitumbua kimeingia mchanga.
179. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu
jua.
180. Kiwi cha yule ni chema cha; hata
ulimwengu uwishe.
181. Kizuri chajiuza kibaya
chajitembeza.
182. Konzi ya maji, haifumbatiki.
183. Konzo ya maji haifumbatiki.
184. Kosa moja haliachi mke.
185. Kozi mwandada, kulala na njaa
kupenda.
186. Kuagiza kufyekeza.
187. Kuambizana kuko kusikilizana
hapana.
188. Kucha M'ngu si kilemba cheupe.
189. Kuchamba kwingi, kuondoka na
mavi.
190. Kufa kufaana.
191. Kufa kwa jamaa, harusi.
192. Kufa kwa mdomo, mate hutawanyika.
193. Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni
kurudia kosa.
194. Kuishi kwingi, kuona mengi.
195. Kujikwa si kuanguka,bali ni
kwenda mbele.
196. Kujikwaa si kuanguka, bali ni
kwenda mbele.
197. Kukopa harusi kulipa matanga.
198. Kukopa harusi, kulipa matanga.
199. Kuku havunji yai lake.
200. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
201. Kula kutamu, kulima mavune.
202. Kulea mimba si kazi kazi kulea
mwana.
203. Kukopa harusi, kulipa matanga.
204. Kumuashia taa kipofu ni kuharibu
mafuta.
205. Kunako matanga kume kufa mtu.
206. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa
zake.
207. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
208. Kupata si werevu, na kukosa si
ujinga.
209. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
210. Kurambaramba ndio kula, kunenepa
kwake Mola.
211. Kusikia si kuona.
212. Kutangulia si kufika.
213. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
214. Kutu kuu ni la mgeni.
215. Kuugua sio kufa.
216. Kuuliza si ujinga.
217. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya
mchukuzi.
218. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
219. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa
shujaa huenda kilio.
220. Kweli ilio chungu, si uongo ulio
mtamu.
221. Kwenda mbio siyo kufika.
222. Kwenye miti hakuna wajenzi.
223. La kuvunda halina rubani.
224. La kuvunda halina ubani.
225. Lake mtu halimtapishi bali
humchefua.
226. Leo kwako, kesho kwa mwenzio.
227. Leo ni leo asemae kesho ni mwongo.
228. Liandikwalo ndiyo liwalo.
229. Lila na fila hazitangamani.
230. Lipitalo, hupishwa .
231. Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
232. Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
233. Lisilokuwapo moyoni, halipo
machoni.
234. Maafuu hapatilizwi.
235. Macho hayana pazia.
236. Mafahali wawili hawakai zizi
moja.
237. Maiti haulizwi sanda.
238. Maji hayapandi mlima.
239. Maji hufuata mkondo.
240. Maji ukiyavuliya nguo huna budi
kuyaoga.
241. Maji usiyoyafika hujui wingi
wake.
242. Maji ya kifuu, bahari ya chungu.
243. Maji yakijaa hupwa.
244. Maji yakimwagika hayazoleki.
245. Maji yamenifika shingoni.
246. Majuto ni mjukuu.
247. Mali ya bahili huliwa na wadudu.
248. Mama ni mama, hata kama ni
rikwama.
249. Mama nipe radhi kuishi na watu
kazi.
250. Mambo kunga.
251. Manahodha wengi chombo huenda
mrama.
252. Maneno makali hayavunji mfupa.
253. Maneno mazuri humtowa nyoka
pangoni.
254. Maneno si mkuki.
255. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi
kufichika.
256. Masikini akipata matako hulia
mbwata.
257. Masikini haokoti,akiokota huambiwa
kaiba.
258. Masikini na mwanawe tajiri na
mali yake.
259. Maskini hana kinyongo.
260. Mavi usioyala, wayawingiani kuku?
261. Mavi ya kale hayanuki.
262. Mbinu hufuata mwendo.
263. Mbio za sakafuni huishia
ukingoni.
264. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
265. Mchagua jembe si mkulima.
266. Mchagua nazi hupata koroma.
267. Mchagua nazi si mfuaji.
268. Mchakacho ujao,halulengwi na
jiwe.
269. Mchama ago hanyeli,huenda akauya
papo.
270. Mchamba kwingi mara ujitia dole.
271. Mcheka kilema hafi bila kumpata.
272. Mchele mmoja mapishi mengi.
273. Mchelea mwana kulia hulia yeye..
274. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka
matao.
275. Mcheza kwao hutuzwa.
276. Mcheza na tope humrukia.
277. Mchezea mavi, hayaachi kumnuka.
278. Mchezea zuri, baya humfika.
279. Mchimba kisima hungia mwenyewe.
280. Mchonga mwiko hukimbiza mkono
wake.
281. Mchuma janga hula na wakwao.
282. Mchumia juani,hulia kivulini.
283. Mdharau biu, hubiuka yeye.
284. Mdharau mwiba mguu huota tende.
285. Meno ya mbwa hayaumani.
286. Mfa maji haachi kutapatapa.
287. Mfa maji hukamata maji.
288. Mficha uchi hazai.
289. Mfinyazi hulia gaeni.
290. Mfuata nyuki hakosi asali.
291. Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
292. Mgaagaa na upwa hali ugari kande.
293. Mganga hajigangi.
294. Mgema akisifiwa tembo hulitia
maji.
295. Mgeni ni kuku mweupe.
296. Mgeni njoo mwenyeji apone.
297. Mgomba haushindwi na mkunguwe.
298. Mgonjwa haulizwi uji.
299. Miye nyumba ya udongo, sihimili
vishindo.
300. Mjinga akierevuka mwerevu yupo
mashakani.
301. Mjinga mpe kilemba utamuona
mwendowe.
302. Mjumbe hauawi.
303. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
304. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
305. Mkamia maji hayanywi.
306. Mkamia maji hayanywi.
307. Mkataa la mkuu huvunjika guu.
308. Mkataa wengi ni mchawi.
309. Mkataa ya Musa hupata ya Firauna.
310. Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
311. Mkono moja hauchinji ng'ombe.
312. Mkono moja haulei mwana.
313. Mkono mtupu haulambwi.
314. Mkono usioweza kuukata,ubusu.
315. Mkosa kitoweo humangiria.
316. Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu
uchungu.
317. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
318. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
319. Mla cha uchungu na tamu hakosi.
320. Mla kuku wa mwenziwe miguu
humwelekea.
321. Mla mbuzi hulipa ngombe.
322. Mla mla leo mla jana kala nini?
323. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa
nawe.
324. Mlala na maiti haachi kulia lia.
325. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
326. Mlimbua nchi ni mwananchi.
327. Mnyamaa kadumbu.
328. Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu
yake i pale pale.
329. Moja shika, si kumi nenda urudi.
330. Moto hauzai moto.
331. Mpanda farasi wawili hupasuka
msamba.
332. Mpanda ngazi hushuka.
333. Mpanda ovyo hula ovyo.
334. Mpemba akipata gogo hanyii chini.
335. Mpemba hakimbii mvua ndogo.
336. Mpende akupendae asiyekupenda
achana naye.
337. Mpiga ngumi ukuta huumiza
mkonowe.
338. Mpofuka ukongweni,hapotewi na
njia.
339. Msafiri kafiri.
340. Msafiri masikini ajapokuwa
sultani.
341. Msasi haogopi mwiba.
342. Msema kweli hukimbiwa na rafiki
zake.
343. Msema kweli ni mpenzi wa mungu.
344. Msema pweke hakosi.
345. Mshika kisu, hashiki makalini.
346. Mshale kwenda msituni haukupotea.
347. Mshoni hachagui nguo.
348. Msi bahati, habahatishi.
349. Msi mbele, hana nyuma.
350. Msishukuru mja, hamshukuru
Molawe.
351. Msitukane wagema na ulevi
ungalipo.
352. Msitukane wakunga na uzazi
ungalipo.
353. Mstahimilivu hula mbivu.
354. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
355. Mtaka lake hasindwi.
356. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi
msiba.
357. Mtaka unda haneni.
358. Mtaka uzuri hudhurika.
359. Mtaka yote hukosa yote.
360. Mtegemea nundu haachi kunona.
361. Mtegemea nundu, haachi konona.
362. Mtego bila ya chambo, haunasi.
363. Mtembezi hula miguu yake.
364. Mteuzi heshi tamaa.
365. Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
366. Mtondoo haufi maji.
367. Mtoto akililia wembe mpe.
368. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
369. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
370. Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
371. Mtu hujikuna ajipatapo.
372. Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi
amekulani.
373. Mtumai cha ndugu hufa masikini.
374. Mtumi wa kunga haambiwi maana.
375. Mtumikie kafiri upate mradi wako.
376. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
377. Muhitaji khanithi walau kana
rijaali.
378. Muiba yai leo kesho hua mwizi wa
ng'ombe.
379. Mume wa mama ni baba.
380. Mungu hamfichi mnafiki.
381. Mungu si asumani.
382. Muonja asali haonji mara moja.
383. Muuza sanda, mauti kwake harusi.
384. Mvua nguo, huchutama.
385. Mvumbika changa hula mbovu.
386. Mvumbika pevu hula mbivu na
mvumbika changa hula mbovu.
387. Mvumilivu hula mbivu.
388. Mvungu mkeka.
389. Mvunja nchi ni mwananchi.
390. Mvuvi ajuwa pweza alipo.
391. Mwacha asili ni mtumwa.
392. Mwamba na wako hukutuma
umwambiye.
393. Mwamini Mungu si mtovu.
394. Mwana maji wa kwale kufa maji
mazowea.
395. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama
wewe.
396. Mwana simba ni simba.The child of
lion is a lion.
397. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
398. Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka,
zuka naye.
399. Mwanga mpe mtoto kulea.
400. Mwangaza mbili moja humponyoka.
401. Mwanzo kokochi mwisho nazi.
402. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
403. Mwanzo wa ngoma ni lele.
404. Mwapiza la nje hupata la ndani.
405. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
406. Mwenda bure si mkaa bure,huenda
akaokota.
407. Mwenda mbio hujikwa kidole.
408. Mwenda omo na tezi marejeo ni
ngamani.
409. Mwenda pole hajikwai.
410. Mwenda wazimu hapewi panga.
411. Mwenda wazimu hapoi, bali hupata
nafuu.
412. Mwenye haja hwenda chooni.
413. Mwenye kelele hana neno.
414. Mwenye kovu usidhani kapowa.
415. Mwenye kubebwa hujikaza.
416. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
417. Mwenye kuumwa na nyoka akiona
jani hushtuka.
418. Mwenye macho haambiwi tazama.
419. Mwenye mdomo hapotei.
420. Mwenye nguvu mpishe.
421. Mwenye njaa hana miko.
422. Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
423. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
424. Mwenye shoka hakosi kuni.
425. Mwenye tumbo ni tumbole,
angafunga mkaja.
426. Mwenzako akinyolewa wewe tia
maji.
427. Mwibaji na watwana, mlifi ni
mwungwana
428. Mwili wa mwenzio ni kando ya
mwilio.
429. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
430. Mwomba chumvi huombea chunguche.
431. Mwosha hadhuru maiti.
432. Mwosha huoshwa.
433. Mwosha husitiri maiti.
434. Mzaha,mzaha, mara hutumbuka
usaha.
435. Mzazi haachi ujusi.
436. Mzigo usiouweza unaubebea nini?
437. Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia
usufi.
438. Mzika pembe ndiye mzua pembe.
439. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
440. Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja
haviwezi.
441. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
442. Nahodha wengi, chombo huenda
mrama.
443. Nani kama mama?
444. Natuone ndipo twambe, kusikia Si
kuona.
445. Nazi haishindani na jiwe.
446. Nazi mbovu harabu ya nzima.
447. Ndege mjanja hunasa kwanye tundu
bovu.
448. Ndege mwigo hana mazowea.
449. Ndevu sio shani, hata beberu
anazo.
450. Ndondondo si chururu.
451. Ndugu chungu, jirani mkungu.
452. Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
453. Ndugu wakigombana, chukua jembe
ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
454. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
455. Ngoma ivumayo haidumu.
456. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
457. Ngoma ya kitoto, haikeshi.
458. Ng'ombe avunjikapo guu hurejea
zizini.
459. Ng'ombe haelemewi na nunduye.
460. Ngombe wa Maskini hazai.
461. Ngozi ivute ili maji. ( Udongo
upate uli maji )
462. Nguo ya kuazima, Haistiri matako.
463. Nia njema ni tabibu, nia mbaya
huharibu.
464. Nifae na mvua nikufae na jua.
465. Nimekula asali udogoni, utamu
ungali gegoni.
466. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka
pilipili.
467. Nimerejesha kikombe na kisahani
chake.
468. Njia ya muongo fupi.
469. Njia ya mwongo ni fupi.
470. Njia ya siku zote haina alama.
471. Nta Si asali; nalikuwa nazo Si
uchunga.
472. Nyani haoni kundule, huliona la
mwenziwe.
473. Nyani haoni kundule.
474. Nyimbo mbaya haibembelezewi motto
475. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi
ngoma.
476. Nyongeza huenda kwenye chungu.
477. Nyota njema huonekana asubuhi.
478. Nyumba usiyolala ndani huijui ila
yake.
479. Nyumba ya udongo haihimili
vishindo.
480. Nzi kufa juu ya kidonda Si
haramu.
481. Ondoa dari uwezeke paa.
482. Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
483. Padogo pako Si pakubwa pa
mwenzako.
484. Painamapo ndipo painukapo.
485. Paka akiondoka, panya hutawala.
486. Paka hakubali kulala chali.
487. Paka hashibi kwa wali, matilabaye
ni panya.
488. Paka wa nyumba haingwa.
489. Panapo wengi hapaharibiki neno.
490. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
491. Pele hupewa msi kucha.
492. Pema usijapo pema; ukipema Si
pema tena.
493. Penye kuku wengi usimwage mtama.
494. Penye mafundi, hapakosi
wanafunzi.
495. Penye mbaya wako, hapakosi mwema
wako/na mwema wako hakosi.
496. Penye miti hakuna wajenzi.
497. Penye nia pana njia.
498. Penye urembo ndipo penye urimbo.
499. Penye wazee haliharibiki neno.
500. Penye wengi pana mengi.
501. Penye wengi pana Mungu.
502. Pilipili usoila, wewe inakuwashia
nini?
503. Pole pole ndio mwendo.
504. Punde si punde.
505. Pwagu hupata pwaguzi.
506. Radhi ni bora kuliko mali.
507. Radhi za wazee, ni fimbo.
508. Sahani iliyofunikwa, kilichomo
kimesitirika.
509. Sahau ni dawa ya Waja.
510. Samaki mmoja akioza, huoza wote.
511. Samaki mkunje angali mbichi.
512. Shida haina hodi.
513. Shida huzaa maarifa.
514. Shika! Shika! na mwenyewe uwe
nyuma.
515. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
516. Shoka lisilo mpini halichanji
kuni.
517. Si kila king'aacho ni dhahabu.
518. Si kila mwenye makucha huwa
simba.
519. Si Mungu mtupu na mkono wa mtu.
520. Sikio halilali na njaa.
521. Sikio halipwani kichwa. (Sikio
halipiti kichwa).
522. Sikio Ia kufa halisikii dawa.
523. Siri ya mtungi aijuaye ni kata.
524. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa
kiungulia.
525. Siku njema huonekana asubuhi.
526. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo
siku utakayokutana na mkweo.
527. Siku ya kufa nyani, miti yote
huteleza.
528. Siku za mwizi, arobaini
529. Simba mwenda kimya (pole) ndiye
mla nyama.
530. Simbiko haisimbuki ila kwa
msukosuko.
531. Sio shehe bali ni shehena.
532. Siri ya maiti aijuaye muosha.
533. Sitafuga ndwele na waganga tele.
534. Sitapiki nyongo harudi haramba.
535. Subira ni ufunguo Wa faraja.
536. Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu.
537. Sumu ya neno ni neno.
538. Tabia ni ngozi ya mwili.
539. Tamaa mbele, mauti nyuma.
540. Taratibu ndio mwendo.
541. Tawi kavu kuanguka si ajabu.
542. Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe
543. Tonga si tuwi
544. Tunda jema halikawii mtini.
545. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia
nyumba.
546. Ujuzi hauzeeki.
547. Uchungu wa mwana, aujue mzazi.
548. Udongo uwahi ungali maji.
549. Udugu wa nazi hukutania chunguni
(pakachani)
550. Uji hajauonja, tayari
ushamuunguza
551. Ukenda kwa wenye chongo, fumba
lako jicho.
552. Ukimpa shubiri huchukua pima.
553. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka
mkundu.
554. Ukimwamsha alolala utalala weye.
555. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke
kuguguna mfupa.
556. Ukiona kwako kunaungua kwa
mwenzako kunateketea.
557. Ukiona moshi, chini kuna moto.
558. Ukiona neno, usiposema neno,
hutapatikana na neno.
559. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
560. Ukiona zinduna, na ambari iko
nyuma.
561. Ukistahi mke ndugu, huzai nae.
562. Ukitaja nyoka, shika fimbo
mkononi.
563. Ukitaka kula nguruwe, chagua
aliye nona.
564. Ukitaka salama ya dunia, zuia
ulimi wako.
565. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa
nyuma.
566. Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.
567. Ukupigao ndio ukufunzao.
568. Ukuukuu wa kamba Si upya wa
ukambaa.
569. Ulimi hauna mfupa.
570. Ulimi unauma kuliko meno.
571. Ulipendalo hupati, hupata
ujaaliwalo.
572. Ulivyoligema, utalinywa.
573. Umeadimika kama la jogoo.
574. Umegeuka mung'unye waharibika
ukubwani.
575. Umejigeuza pweza, unajipalia
makaa?
576. Umekuwa bata akili kwa watoto?
577. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
578. Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
579. Umoja ni nguvu na utengano ni
udhaifu.
580. Unajenga kwa mwenzio na kwako
kunaporomoka!!
581. Unakuja juu kama moto wa kifuu.
582. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha
kuku.
583. Ungalijua alacho nyuki,
usingalionja asali.
584. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa
usijiachie).
585. Usiache kunanua kwa kutega.
586. Usiache mbachao kwa msala upitao.
587. Usiache tawi kabla ya kushika
tawi.
588. Usiandikie mate na wino ungalipo
589. Usicheze na simba, ukamtia mkono
kinywani.
590. Usijifanye kuku mweupe.
591. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye
meno
592. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
593. Usilolijua ni sawa na usiku wa
giza.
594. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na
mwezi.
595. Usiniache njia panda.
596. Usinikumbushe kilio matangani.
597. Usinipake mafuta kwa nyuma ya
chupa.
598. Usinivishe kilemba cha ukoka.
599. Usione simba kapigwa na mvua.
600. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
601. Usisafirie nyota ya mwenzio.
602. Usisahau ubaharia kwa sababu ya
unahodha.
603. Usishindane na Kari; Kari ni mja
wa Mungu.
604. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
605. Usitukane wakunga na uzazi
'ungalipo.
606. Utakosa mtoto na maji ya moto.
607. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
608. Utaula na chua kwa uvivu wa
kuchagua.
609. Vita havina macho.
610. Vita si lele mama.
611. Vita vya panzi, neema ya kunguru
612. Waarabu wa pemba, hujuana kwa
vilemba
613. Wache waseme.
614. Wafadhilaka wapundaka.
615. Wagombanao ndio wapatanao.
616. Watu wanahisabu nazi, wewe
unahisabu makoroma.
617. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo
ni nyasi.
618. Watetea ndizi, mgomba si wao.
619. Wazuri haweshi.
620. Wema hauozi..
621. Wengi wape.
622. Wingi si hoja.
623. Zinguo la mtukufu, ni ufito.
KUHUSU SISI
JINA
LA KAMPUNI: FULLBRIGHT EDUCATION CENTRE
MAHALI:
MNAZIMMOJA, LINDI, TANZANIA.
SIMU:
+255658218136/ +255624318136.
HUDUMA ZETU:-
1.
KOZI YA
KOMPYUTA {coming soon}
2.
KOZI YA
KIINGEREZA,
3.
KOZI YA PRE
FORM 1 & 5,
4.
ELIMU YA
SEKONDARI KWA MIAKA MIWILI {QT},
5.
KURUDIA MTIHANI
{form 4 & 6},
6.
MASOMO YA ZIADA
{TUTION} KWA;
i)
CHEKECHEA &
SHULE ZA MSINGI{DARASA LA 1-7},
ii)
SEKONDARI:
KIDATO CHA 1-4 {arts
& science},
iii)
SEKONDARI:
KIDATO CHA 5&6 {arts & science}.
VITABU VYETU:-
1.
ALPHABET AND
NUMBER BOOK,
2.
CONJUGATION OF
THE 1000 ENGLISH VERB{with Swahili translation},
3.
ENGLISH TENSES
{primary & secondary students},
4. PARTS OF SPEECH,
5. O-LEVEL PRACTICLE